×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto atofautiana na kauli kuwa Kenyatta analenga kusalia uongozini

Ruto atofautiana na kauli kuwa Kenyatta analenga kusalia uongozini

Kwa mara ya kwanza Naibu wa Rais, William Ruto ametofautiana na wandani wake wanaosema kwamba Rais Uhuru Kenyatta analenga kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake kukamilika mwaka wa 2022.

Kwa mujibu wa Ruto, Rais Kenyatta ni kiongozi anayependa demokrasia na kamwe hawezi kufanya hivyo kwa kuwa katiba haimruhusu.

Ruto amewataja viongozi hao kuwa wanafiki na wanaoendeleza propanganda na kuwa Rais mwenyewe hajawahi kutamka kuhusu kuendelea kusalia mamlakani.

Akizungumza kwenye mkutano na viongozi wa Jamii za Luo vilevile Abaluhyia nyumbani kwake katika eneo la Kareni, Ruto aidha amesisitiza haja ya kuwapo kwa uwazi na kujumuishwa kwa viongozi wote katika mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho.

Kwa upande wao viongozi waliokuwa wameandamana na Ruto, akiwamo aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama, aliyekuwa seneta wa Kakemga Bony Khalwale vilevile Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua wamesema wataunga mkono mapendekezo ya BBI iwapo yatakuwa yenye kuwanufaisha Wakenya.


Aidha aliyekuwa mgombea wa kiti cha Ubunge kwenye eneo bunge la Kibra wa ANC Eliud Owalo ambaye amehamia rasmi kwenye ngome ya Naibu wa Rais amesisitiza kwamba amefanya hivyo kwa kuwa Ruto ni kiongozi aliye na maono.