×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya yarekodi visa 48 vya korona

Kenya yarekodi visa 48 vya korona

Kwa kipindi cha siku kumi na moja sasa Kenya imeendelea kurekodi maambukizi ya chini kwa asilimia 6.1 huku kukiwa na matumaini ya kukabiliwa kabisa kwa janga la korona iwapo taifa litaendele kuripoti chini ya asilimia tano ya maambukizi kwa majuma mawili.

Chini ya kipindi cha saa ishirini na nne zilizozipita watu arubaini na wanane wamekithibitishwa kuambukizwa kutokana na sambuli 1,081, Idadi hii ikiwa ya chini kwa kipindi cha miezi mitatu,

Watu hao 48 sasa wanafikisha idadi juma ya watu 36,205  ambao wameambukizwa virusi vya korona humu nchini.

Akizungumza wakati wa kutoa takwimu za maambukizi ya kila siku, Katibu wa Utawala katika Wizara ya Afya Dakta Mercy Mwangangi amesema kuwa walioambukizwa wote ni Wakenya huku 31 wakiwa wanaume na 17 wakiwa wanawake. Watu hao aidha wanajumuisha mtoto mwenye umri wa miaka kumi na miwili na mzee  wa miaka sabini na mitano.

Kaunti ya Mombasa leo hii inaongoza kwa visa vya maambukizi baada ya watu 20 kuambukizwa ikifuatwa na Nairobi na visa kumi na vitano, Tharaka Nithi vinne, Kiambu na Kilifi viwili viwili, Machakos, Wajiri na Homabay zikiwa na kisa kimoja kimoja.

Mwangangi ameonya kuhusu kuendelea kuongezeka kwa maambukizi katika Kaunti ya Mombasa.

Afueni ni kwamba watu 176 wamepona , 45 wakiwa waliohudumiwa nyumbani huku 131wakiwa wale waliokuwa wakihudumiwa hospitalini na kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa watu kuwa 23, 244.

Hata hivyo, watu wengine wawi wamethibitishwa kufariki dunia na kufikisha 624 idadi jumla ya vifo vya korona.

Katika kuimarisha vita dhidi ya korona Mamlaka ya Huduma za Jiji NMS kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Nairobi imewapa mafunzo wahudumu wa afya vijijini 1,500 na kuimarisha miudo msingi katika hospitali mbalimbali ili kukabili janga la korona.

Serikali kwa mara nyingine imeonya kuhusu kuendela kupuuzwa kwa maagizo ya kujilinda na kuwataka Wakenya kujilinda.