×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sudi ashtakiwa kwa matamshi ya uchochezi

Sudi ashtakiwa kwa matamshi ya uchochezi

Mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi amefikishwa katika Mahakama ya Nakuru ambapo amefunguliwa mashtaka ya uchochezi.

Sudi amekesha katika KItuo cha Polisi cha Central mjini Nakuru baada ya kujiwasilisha katika Kituo cha Kapsaret kwenye Kaunti ya Uasin Gishu. Baadaye Sudi alisafirishwa hadi Nakuru akiandamana na mawakili wake Gladys Boss Shollei ambaye vilevile ni Mwakilishi wa Kike wa Uasin Gishu na Isaac Terer.

Sudi anatuhumiwa kutoa matamshi ya uchochezi vilevile kumkosea heshima Rais Uhuru Kenyatta na familia yake. Ikumbukwe viongozi mbalimbali nchini hasa akina mama wamekuwa wakiendeleza maandamano nchini kumtaka Sudi kuomba msamaha kwa kumkosea heshima Rais Kenyatta.

Hata hivyo, Sudi tayari alisema kamwe hataomba msamaha kwani hakusema lolote la kumkosea hehsima rais na familia yake.

Wiki iliyopita, mwenzake wa Emurua Dikirr, Johana Ng'eno alifikishwa katika mahakama hiyo ambapo alishtakiwa kwa makosa sawa na yake. Baadaye aliachiliwa kwa dhamana ya hsilingi milioni moja pesa taslimu.