×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amekana mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amekana mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amekana mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi. Akiwakilishwa na wakili wake Cecil Miller na George Kithi, Sonko amekana mashtaka hayo anayodaiwa kutumia mamlaka yake kujinufaisha na shilingi milioni kumi kutoka kwa kampuni moja.

Wiki jana , Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Douglas Ogoti alimwagiza Sonko kufika mbele ya Mahakama ya Ufisadi na kukabiliwa na mashtaka mapya. Agizo hilo lilitolewa baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji kumfungulia mashtaka hayo.

Kwenye mashtaka hayo, Sonko anadaiwa kuwa mnamo mwezi Januari mwaka jana alitumia jina la ofisi yake kujipatia shilingi milioni kumi kutoka kwa Kampuni ya Web Tribe Limited kupitia kampuni ya ulinzi ya ROG Security Limited.

Mashtaka mengine yaliyojumuishwa kwenye kesi ya leo, ni utakatishaji wa fedha yaani Money Laundering, vilevile kujipatia mali kupitia njia za kihalifu, mashtaka ambayo Sonko ameyakana yote.