×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Gavana wa Garissa Ali Korane ahojiwa kuhusu madai ya ufisadi wa shilingi milioni 233

Gavana wa Garissa Ali Korane ahojiwa kuhusu madai ya ufisadi wa shilingi milioni 233

Gavana wa Garissa Ali Korane angali anahojiwa katika Makao Mkuu ya Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC kuhusu utumuzi mbaya wa ufadhili wa shilingi milioni 233 zilizotengewa miradi ya maendeleo kwenye kaunti yake.

Korane alijiwasilisha katika ofisi za EACC mapema leo baada ta Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji kuagizwa kukamatwa kwake pamoja na maafisa wengine wanne wa kaunti hiyo kufuatia madai ya wizi wa fedha hizo.

Korane ambaye anahudumu kwa muhula wa kwanza katika wadhifa wa gavana anashutumiwa kutumia vibaya ufadhili uliotolewa na Benki ya Dunia. Fedha hizo zililenga kujengwa kwa soko jipya, kukarabatiwa kwa barabara mjini garissa na kutenga maeneo ya watu kupitia, suala ambalo hakijafanyika tangu mweze Februari mwaka uliopita.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Haji alisema kwamba ameikabidhi kesi hiyo kwa waendesha mashtaka wenye tajriba na kujiondoa kwenye mchakato huo kwani uchunguzi huo unaihusisha kaunti ambayo yeye ni mzaliwa.

Miongoni mwa watakaofunguliwa mashtaka pamoja na Gavana huyo ni Ofisa Mkuu wa Idara ya Fedha Ibrahim Malow, Mkuu wa Hazina ya Kaunti hiyo Mohammed Abdulahi, mwenzake Abdi Shale na mkuu wa Idara ya Uhasibu Ahmed Aden.