×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Washikadau wa elimu wapewa jukumu la kutoa mapendekezo kuhusu kurejelewa kwa shughuli za masomo

Washikadau wa elimu wapewa jukumu la kutoa mapendekezo kuhusu kurejelewa kwa shughuli za masomo

Washikadau mbalimbali wa Idara ya elimu wametwikwa jukumu la kujadiliana na kutoa mapendekezo ya ni lini shughuli za masomo zitarejelewa baada ya kusitishwa kuanzia mwezi Machi mwaka huu.

Akidokeza haya baada ya mkutano huo uliofanyika katika Taasisi ya Ukuzaji Mtalaa KICD hapa jijini Nairobi, Magoha amesema kwamba washika dau hao watajadiliana mikakati inayopaswa kuzingatiwa kabla ya kurejelewa kwa masomo nchini pamoja na kuishauri wizara yake kuhusu masuala yanayohusu ufunguzi wa shule.

Wakati uo huo, Magoha amepuuza taarifa kwamba walimu halali walioajiriwa na bodi za shule, BOM, hawajapokea mishahara yao akisisitiza kwamba fedha hizo zilitumwa zaidi ya wiki sita zilizopita.

Miongoni mwa waliotwikwa jukumu hilo ni Mwenyekiti wa Kamati maalumu iliyobuniwa kubuni kanuni za kuzingatiwa wakati wa kufungua taasisi za elimu Dkt. Sarh Ruto, makatibu wa Wizara ya Elimu, viongozi wa Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT, Chama cha Walimu wa Vyuo vya Kadri na Shule za Upili KUPPET, Chama cha Wazazi PA pamoja na wawakilishi wa Tume ya Huduma za Walimu TSC.

Hata hivyo, baadhi ya walimu wameiambia Radio Maisha kwamba hawajapokea mishahara yao. Hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

Tomkins Barasa: Magoha anasema bonafide BOM teachers wamelipwa.Kwani Wengine si bonafide ;NI BONFACE  NA BONVENTURE

Jasper Ondimu: Apart from chest thumbing and lying, Magoha hasn't said anything important today.

Jamaa kwa jina Elite Kenyan: Kwani wengine wanani Huduma namba au Hamna aliyelipwa. Huu ujinga wa kuchezea akili za wakenya atakoma kama alivyokoma la mamake.

Bwalimu Chebisa: None has been paid as far as I know.