×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shirika la Green Africa Foundation lahimiza umuhimu wa upanzi wa miti

Shirika la Green Africa Foundation lahimiza umuhimu wa upanzi wa miti

Katika kuhimiza upanzi wa miti na umuhimu wake, Shirika la Green Africa Foundation limeandaa hafla inayowashirikisha washikadau mbalimbali ili kufanikisha lengo hilo. Halfa ya uhamasisho huo hufanyika tarehe kama ya leo, yaani Septemba 14 kila mwaka.

Hafla ya mwaka huu imefanyika kwenye eneo la Nkaimurunga, Ongata Rongai katika Kaunti ya Kajiado, chini ya kaulimbiu ya ‘plant your age’, yaani kupanda miti sawasawa na umri wao, mfano ukiwa na umri wa miaka 30, uhahimizwa kupanda miti 30. Lengo aidha ni kuwahamasisha watu umuhimu wa miti kwa uhai wa mwanadamu, mfano kuvutia mvua, hewa safi, mvuto wa mazingira na kadhalika.

Masuala mengine yanayosisitizwa katika siku hii ya ‘plant your age’ ni umuhimu wa kuimarisha afya zatu kupitia lishe bora na mazoezi ya mara kwa mara, kuimarisha uhusiano kupitia mawasiliano bora na kusafiri pamoja na kuchangia amani miongoni mwa jamii. Aidha, kuna masuala ya kuanzisha biashara na fursa za kazi.

Siku hii pia hutumiwa kukumbuka juhudi za waliojitojea kupigania mazingira, mfano Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Lobel, Marehemu Wangari Maathai na aliyekuwa Rais wa tatu wa Kenya, Mwai Kibaki kupitia mpango wa Mwai Kibaki Green Corner uliohusu upanzi wa miti.