×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mbunge wa Kapsaret Oscur Sudi ameenda mafichoni baada ya maafisa wa polisi kupiga kambi katika boma lake usiku kucha wakipanga kumkamata

Mbunge wa Kapsaret Oscur Sudi ameenda mafichoni baada ya maafisa wa polisi kupiga kambi katika boma lake usiku kucha wakipanga kumkamata

Mbunge wa Kapsaret Oscur Sudi ameenda mafichoni baada ya maafisa wa polisi kupiga kambi katika boma lake usiku kucha wakipanga kumkamata kwa tuhuma za kutoa matamshi ya chuki na uchochezi.

Aidha, watu watatu wameripotiwa kujeruhiwa baada ya mamia ya wakazi kukabiliana na maafisa wa polisi waliotaka kumkamta Sudi wakati wa usiku wa kuamkia leo.

Wakazi hao walikita kambi kwa Mbunge huyo wakisema wasingeruhusu Sudi kukamatwa kwa kosa ambalo hawakuwa wamefahamishwa.

Vilevile viongozi waliojumuika na wakazi hao akiwamo Mwakilishi wa Kike wa Uasin Gishu Gladys Sholei, wamewakosoa polisi wakisema wangemwagiza Sudi ajiwasilishe kwao badala ya kuvamia makazi yake wakati wa usiku.

Mwengine ambaye amekashifu kisa hicho ni Naibu Katibu wa Chama cha Jubilee Caleb Kositany ambaye amesema ni kinaya kwamba baadhi ya wakosoaji wa Naibu wa Rais William Ruto wamekuwa wakimtusi bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Akizungumza katika Kijiji cha Lolkiringeet katika Eneo la Kiminini kwenye Kaunti ya Trans Nzoia, Kositany ambaye pia ni Mbunge wa Soy ameihimiza Idara ya Polisi kutekeleza wajibu wake bila ubaguzi

Kwa upande wake Mbunge wa Kimilili, Didimus Barasa amesema Sudi ni kiongozi ambaye alifaa kuagizwa na maafisa wa polisi kujiwasilisha kwao badala ya kuzua taharuki.

Mapema leo Rais wa Chama cha Wanasheria nchini, LSK Nelson Havi ameshtumu namna maafisa wa polisi walivyofurika usiku nyumbani kwa Sudi kwa nia ya kumkamata.

Kupitia mtandao wake wa twitter, Havi amesema makosa ambayo Sudi anatuhumiwa kuhusika hayatoshi kumchukulia hatua kama mtu aliyehusika katika wizi.