×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila aendelea kuupigia debe mpango wa BBI katika eneo la Pwani

Raila aendelea kuupigia debe mpango wa BBI katika eneo la Pwani

Kinara wa ODM Raila Odinga ameendelea kupigia debe Mpango wa Upatanishi BBI akisema ndiyo suluhu pekee ya utata wa uongozi katika taifa hili.

Akizungumza Jijini Mombasa wakati wa ziara yake muda mfupi uliopita, Raila amesema BBI itaangazia masuala mbalimbali yakiwamo maslahi ya kina mama na hata kuboresha ugatuzi.

Akirejelea suala la mkwamo wa mfumo mpya wa ugavi wa fedha za kaunti katika Bunge la Seneti kwa miezi miwili sasa, Raila ambaye awali alipinga mfumo huo kabla ya kuunga mkono, amesema BBI itatoa suluhu ya kudumu kwenye mgao wa mapato ya serikali kwa kaunti.

Raila kwa mara nyingine amewakashifu wanasiasa wa mrengo wa Naibu wa Rais William Ruto, ambao wanapinga BBI, akisisitiza kwamba yeye na Rais Uhuru Kenyatta hawalengi kujitafutia nafasi za uongozi ifikapo mwaka wa 2022.

Ametumia fursa hiyo kutetea suala la kuongeza nyadhifa za waziri mkuu na manaibu wake wawili serikalini, akisema hautakuwa mzigo kwa Mkenya mlipa kodi jinsi inavyodaiwa na wandani wa Ruto.

Ikumbukwe Ruto na washirika wake wamekuwa wakipinga ushirikiano wa Rais Kenyatta na Raila maarufu Handshake tangu mwezi machi mwaka wa 2018, kwa misingi kwamba wawili hao wanalenga kujinufaisha kisiasa kwa kujitafutia nafasi za uongozi kwa kisingizio cha kuwaunganisha Wakenya.