×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Polisi wakita kambi nyumbani kwa mbunge Oscur Sudi ili kumkamata kwa madai ya uchochezi

Polisi wakita kambi nyumbani kwa mbunge Oscur Sudi ili kumkamata kwa madai ya uchochezi

Kizaa zaa kimeshuhudiwa usiku wa kuamkia leo wakati polisi walipofika nyumbani kwa Mbunge wa Kapsaret, Oscur Sudi kumkamata kwa kuendeleza matamshi ya uchochezi na kumkosea heshima Rais Uhuru Kenyatta na familia yake. Inaarifiwa baadhi ya vijana waliifunga kwa muda barabara inayoelekea nyumbani kwa Sudi ili kuwazuia polisi kuelekea huko. Walisisitiza kwamba hawataruhusu mbunge wao kukamatwa usiku. Hivi ndivyo hali ilivyokuwa nyumbani kwa Sudi.

Wakili wa Sudi, Glady Sholei ambaye pia ni Mwakilishi wa Kike katika Kaunti ya Uasin Gishu amemtetea mteja wake huku akisema polisi hawakufa na haki ya kumfumania nyumbani kwake usiku ili kumkamata. Sholei alikuwa akizungumza na wanahabari usiku wa kuamkia leo nyumbani kwa Sudi.

Hatimaye polisi waliondoka nyumbani kwa mbunge huyo bila kumkamata. Awali Sudi alifanya maandamano ya amani na wafuasi wake mjini Eldoret ambapo aliendelea kupuzilia mbali wito wa wanaomtaka kujiuzulu na kumwomba Rais Kenyatta na mamaye msamaha kwa kutoa matamshi ya kuwadhalilisha.

Wakati uo huo mwenzake wa Emurua Dikir Johana Ng'eno ambaye pia anahusishwa na tuhuma za uchochezi, alikaribishwa nyumbani kwake baada ya kuachiliwa na mahakama kwa dhamana. Hata hivyo makabiliano yalishuhudiwa baina ya polisi na wafuasi wake waliojitokeka kwa wingi kumkaribisha. Ng'eno alisisitiza kwamba hatasita kuzungumzia suala lolote lile kuhusu serikali iwapo haridhiki na namna nchi inavyoendeshwa.