×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Zaidi ya watoto 3,500 huthibitishwa kuwa na saratani kila mwaka

Zaidi ya watoto 3,500 huthibitishwa kuwa na saratani kila mwaka

Mwezi Septemba hutengwa kuadhimisha saratani inayowaathiri watoto na kuwakumbuka watoto waliofariki kutokana na ugonjwa huo huku mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo ikiendelea. Maadhimisho haya ni miongoni mwa maadhimisho mengine ya magonjwa yasiyoambukiza mfano Kisukari na shinikizo a damu mwilini.

Nchini Kenya Zaidi ya watoto 3,500 huthibitishwa kuwa na saratani kila mwaka, idadi hiyo inaamika kuwa ya juu Zaidi ikizingatiwa visa vingi huwa haviripotiwi rasmi. Vilevile asilimia 80 ya watoto walio na saratani hufariki ikilinganishwa na mataifa yalioyoendelea ambapo asilimia 80 hudhibiti ugonjwa huo.

Utafiti unabainisha kwamba idadi hiyo ya juu ya vifo imechangiwa pakubwa na ukosefu wa uhamasisho, ugonjwa kutambulika ukiwa katika awamu ya mwisho, ukosefu wa mbinu mwafaka za matibabu na gharama ya juu ya matibabu.

Vilevile imebainika kwamba asilimi 1 pekee ya watoto walio na saratani nchini hupata huduma ya kupunguza maumivu na kushughulikiwa na wataalam wa afya vilivyo wakati ugonjwa huo ukiwa katika awamu ya mwisho yaani palliative care, kumaanisha asilimia 99 ya watoto ambao hawana uwezo huo hufariki wakiwa na uchungu mno.

Hata hivyo,Shirika la Afya Duniani WHO, mwaka wa 2018 lilitangaza kuweka mikakati ya kuhakisha asilimia 60 ya watoto walio na saratani wanaudhibiti ugonjwa huo ifikapo mwaka 2020.