×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

COVID-19 imesaidia pakubwa katika kuweka wazi mianya ilioko katika sekta ya afya nchini

COVID-19 imesaidia pakubwa katika kuweka wazi mianya ilioko katika sekta ya afya nchini

Tangu kuanza kwa janga la COVID-19 ilibainika kuwa waliokuwa na magonjwa sugu walikuwa katika athari ya kuambukizwa virusi vya korona kwa urahisi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni yasiyoambukiza yaani Non Communicable diseases NCDs mfano Kisukari, Shinikizo la damu mwilini na saratani. Wiki hii Kenya imejiunga na mataifa mengine kuadhimisha na kuelimisha kuhusu magonjwa hayo kwa kampeni iitwayo Global Week of Action. Mwanahari wetu wa Masuala ya Afya Rosa Agutu amezungumza na  na kuandaa taarifa hiyo.

Magonjwa yasiyoambukiza yaani Non Communicable diseases NCDs yanasababisha asilimia 70 ya vifo duniani kila mwaka. Vyanzo vikuu vya magonjwa hayo ni utumiaji wa tumbaku, kula vyakula vinavyokosa virutubishi vyote, kutofanya mazoezi mara kwa mara, utumiaji mbaya wa pombe na uchavuzi wa hewa.

Kwa mujibu wa Catherine Karekezi,Mshauri katika Chama cha Kitaifa cha Magonjwa yasiyo ya ambukiza NCD Alliance of Kenya, janga la COVID-19 limesaidia pakubwa katika kuweka wazi mianya ilioko katika sekta ya afya nchini, kwani wagonjwa wengi wameathirika tangu kutangazwa kwa kisa cha kwanza cha virusi vya korona nchini.

Karekezi vilevile anaeleza kuwa katika hotuba ya kila siku ya Wizara ya Afya walio na magonjwa sugu hasa yasiyoambukizwa walishauriwa mara kwa mara kuwa makini ila Wizara hiyo haikuweka mikakati ya kuboresha huduma zao wanapokwenda hospitalini.

Anasema baadhi ya changamoto walizopitia wagonjwa wa NCDs hasa wakati kulikuwa na marufuku ya usafiri hadi kwenye kaunti nyingine zilizokuwa na idadi ya juu ya maambukizi ya korona ni  kushindwa kusafiri kupata matibabu katika hospitali za rufaa zilizoko katika kaunti hizo. Aidha wengine walikosa namna ya kulipia huduma za matibabu baada ya kusimamishwa kazi.

Karekezi amesema hata baada ya baadhi ya hospitali kurudia hali ya kawaida hofu ni kwamba kunaweza kushuhudiwa idadi ya juu ya madhara ya baadaye yaliyosababishwa na kuchelewa kupata huduma za matibabu. Mfano mtu aliye na kisukari akikosa matibabu ya haraka na kudhibiti ugonjwa huo anaweza kuwa na matatizo ya figo huku wa shinikizo la damu mwilini akihofiwa kupata kiarusi yaani stroke.

Miongoni mwa matakwa yaliyopendekezwa kuhakikisha walio na maradhi hayo wanashughulikiwa vilivyo hasa wakati huu wa janga la COVID-19 ni kuwapa mafunzo wahudumu wa afya kuhusu NCDs na kuhakikisha matakwa yao pia yanafanywa kipaumbele wakati huu wa janga la COVID-19.

Vivile,mazingira yawe salama wagonjwa wanapoenda kupata huduma za afya na kusisitiza kukumbatiwa kwa mfumo wa kupata huduma za afya kupitia mtandao.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani mwaka 2015 magonjwa yasiyoambukizwa yamesababisha asilimia 31 ya vifo nchini huku asilimia 51 ya vifo vikiwa vya watu waliochini ya miaka 70. Vilevile zaidi ya asilimia 40 ya wanaolazwa hospilini ni walio na magonjwa yasiyoambukizwa huku magonjwa hayo yakisababisha asilimia 40 ya vifo hospitalini.