×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 212 waambukizwa Korona, 4 wakifariki Kenya

Watu 212 waambukizwa Korona, 4 wakifariki Kenya

Watu 212 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona kwa kipindi cha saa 24 zilizopita baada ya sampuli 3, 037 kipimwa.

Idadi jumla ya walioambukizwa Korona kufikia sasa ni 34, 704.

Katibu wa Utawala katika Wizara ya Afya Dkt. Rashid Aman ametoa ripoti hiyo akiwa Kaunti ya Homa Bay ambapo alizindua kituo cha kutibu na kushughulikia wagonjwa Malaria.

Vilevile, watu 195 wamepona, miongoni mwao 141 walikuwa karantini nyumbani huku 54 wakiwa waliokuwa katika hospitali mbalimbali nchini.

Waliofariki kufikia sasa kutokana na Ugonjwa wa COVID - 19 ni 585, ambapo watu wanne wamethibitishwa kufariki Alhamisi.