×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sikulazimswa, asema Manjari akidili kauli kauli kuhusu yaliyofanyika KEMSA

Sikulazimswa, asema Manjari akidili kauli kauli kuhusu yaliyofanyika KEMSA

Afisa Mkuu Mtendaji wa Mamlaka ya Usambazaji wa Vifaa vya Matibabu KEMSA Jonah Manjari sasa amebadili kauli yake ya awali na kusema hakuna afisa yeyote aliyeshinikizwa katika KEMSA kutoa tenda kwa kampuli fulani.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Kitaifa ya Afya, Manjari ambaye awali alisema Waziri wa Afya Mutahi Kagwe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Susan Mochache walimpa maelekezo kuhusu ununuzi wa vifaa vya matibabu, amesema hakulazimishwa kupendelea kampuni fulani wakati wa kutoa tenda.

Manjari amesema hakufanya kazi chini ya shinikizo la watu wenye ushawishi serikalini na kwamba kila hatua alizochukua ziliwiana na majukumu yake katika KEMSA.

Manjari ametumia fursa hiyo kusisitiza kauli ya Waziri Kagwe kwamba hakuna fedha zilizopotea wala kuibwa kutokana na mipango ya Kukabili Janga la Korona.