×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mvutano zaidi kushuhudiwa katika Bunge la Seneti

Mvutano zaidi kushuhudiwa katika Bunge la Seneti

Na caren Papai,

NAIROBI, KENYA, Mvutano zaidi unatarajiwa Jumanne katika Bunge la Seneti baada ya kundi la Maseneta wanaopinga mfumo unaopendekezwa na Tume ya Ugavi wa Mapato CRA, kutishia kueleka Mahakamani iwapo mfumo huo utapitishwa.

Tayari mchakato wa Kiranja wa Seneti Irungu Kang'ata kuwashawishi maseneta kuunga mkono mfumo huo umepata pigo baada ya kikao cha jana katika Kaunti ya Kiambu kutibuka. Mkutano huo ulisitishwa kufuatia taarifa kwamba waliothibitisha kuuhudhuria asilimia 70 ni wale wanaopinga mfumo wa CRA na hivyo basi hakungekuwa na maridhiano.

Hata hivyo, Kang'ata amesema kuwa Jumatatu ataongoza Kamukunji nyingine kabla ya vikao vya kesho ambapo mapendekezo mbalimbali ya Maseneta yatajadiliwa.

Kundi hilo chini ya Vuguvugu la One Kenya Movement, limesema kuwa Wakenya hawajashirikishwa kutoa maoni yao katika mfumo ambao unaopendekeza Serikali za Kaunti kupewa mgao kwa kuzingatia idadi ya watu.

Maseneta hao wanaounga mkono marekebisho katika mswada huo, anavyopendekeza Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja, wamesema wataendelea kusimama kidete kupigania haki ya Wakenya. Ledema Ole Kina ni Seneta wa Narok ambaye tayari amefutilia mbali mkutano wa Kang'ata.
 
Jumanne, kwa mara ya nane, Seneti itajadili mswada huo wa CRA wakati Magavana wakiendelea kulalamikia kucheleweshwa kwa fedha za maendeleo. Wamesema hatua hiyo imetatiza utaoaji huduma kwa  kaunti na shughuli za maendeleo.