array(0) { } Radio Maisha | Wakazi wa Makueni ni wenye furaha -Infortrak
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakazi wa Makueni ni wenye furaha -Infortrak

Wakazi wa Makueni ni wenye furaha -Infortrak

Kaunti ya Makueni ndio yenye idadi kubwa ya watu wenye furaha tele kuliko maeneo mengine nchini Kenya.

Utafiti wa hivi punde wa Shirika la Infotrak umeonesha hivyo.

Utafiti huo umeonesha kwamba kaunti ya Makueni imeongoza kwa asilimia 64. 4 ya watu wenye furaha, ikifuatwa na Pokot Magharibi kwa asilimia 62. 4, kisha Machakos kwa asilimilia 62.1 huku Bomet ikiwa na asilimia 61.8.

Aidha, Kwale imekuwa kaunti ya tano yenye watu wa furaha kwa kuwa na asilimia 61.3.

Kaunti nyingine ambazo ziko katika kumi bora ya watu wenye furaha ni ikiwamo Elgeyo Marakwet, Marsabit, Uasin Gishu, Kericho na Mandera.

Hata hivyo, watu wanaoshi jijini Nairobi, wameorodheshwa wa mwisho kabisa kuwa na furaha kwa kuwa kaunti ya arubaini na saba kwenye utafiti huo.

Kisumu imekuwa nambari 24 huku Mombasa ikiwa ya 44.

Infrotrak imefanya utafiti huo miezi michache tu baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa UN kuitaja Kenya kuwa miongoni mwa mataifa ya watu wenye furaha zaidi katika Bara la Afrika.

UN ilitaja Kenya kuwa taifa la

Kenya iliorodheshwa kuwa taifa la 121 ya watu wenye furaha miongoni mwa mataifa 153 yaliyohusishwa kwenye utafiti huo wa mwezi Machi mwaka huu.Uganda ilikuwa nambari 126, Burundi ikawa nambari 140, Tanzania nambari 148 huku Rwanda ikiwa ya 150.

Hata hivyo, taila la Sudan liliorodheshwa kuwa taifa ambalo wananchi wake hawana furaha kabisa katika Ukanda wa Afrika Mashariki.