array(0) { } Radio Maisha | Marekani yaiorodhesha Kenya kuwa miongoni mwa mataifa yasiyo salama kuafuatia korona
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Marekani yaiorodhesha Kenya kuwa miongoni mwa mataifa yasiyo salama kuafuatia korona

Marekani yaiorodhesha Kenya kuwa miongoni mwa mataifa yasiyo salama kuafuatia korona

Taifa la Marekani limewatahadharisha raia wake dhidi ya kusafiri kuja humu nchini kufuatia kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya Virusi vya korona.

Taarifa kutoka ubalozi wa Marekani inaeleza kwamba Kenya iliondoa marufuku ya kusafiri hata nje ya chi na kurejelea shughuli za kawaida, hivyo kuiorodhesha Kenya kuwa taifa la daraja ya tatu yaani Level 3 katika tishio la afya.

Kulingana na Baraza la Kudhibiti maambukizi ya Magonjwa nchini Marekani CDC , Level 3 inamaanisha kwamba ni hatari huku raia wake wakishauriwa kutosafiri kabisa.

Notisi hiyo imewashauri raia wake kwamba hakuna mipango iliyowekwa kuwahakikishia usalama wao, ikisema uwezekano wa kuambukizwa korona nchini humu uko juu zaidi, sawa na mataifa mengine mia mbili na manane ambayo yameorodheshwa.

Kando na hayo inaonya kwamba watakaosafiri kuja nchini humu kisha kuugua basi huenda wasipate huduma za afya zinazostahili.

Mataifa mengine Barani Afrika ambayo Marekani imeweka katika Level 3 ni, Rwanda, Tanzania,  Sudan Kusini, Ethiopia, Djibouti, Uganda, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe miongoni mwa mengine.

Leo hii visa vya korona nchini humu vimefikia elfu ishirini na sita, mia nne thelathini na sita baada ya watu mia tano tisini na tsia zaidi kuthibitishwa kuambukizwa.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa vifo vimefikia mia nne ishirini baada ya watu wengine wawili kufariki dunia.

Marekani ambayo ndiyo imeaathirika zaidi Duniani kote kutokana na Korona, ina zaidi ya watu milioni tano waliaombukizwa korona na wengine zaidi ya elfu mia moja sitini ambao wamefariki dunia.