×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Taasisi za elimu zitafunguliwa Januari 2021 -George Magoha

Taasisi za elimu zitafunguliwa Januari 2021 -George Magoha

Mpango wa kufunguliwa kwa taasisi za elimu mapema mwakani ungalipo. Amesema Waziri wa Elimu profesa George Magoha .

Akizungumza mjini Kisumu, alipoandamana ana Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, Waziri Magoha hata hivyo amesisitiza kwamba taasisi hizo zitafunguliwa tu iwapo maambukizi ya korona, yatapungua nchini.

Amewashtumu wanaoshinikiza shule kufunguliwa haraka, akisema zitasalia kufungwa kwa ajili ya usalama wa kila Mkenya, akisema ukaguzi wa taaissi zote unaendelea kuhakikisha zote zinafuata masharti yaliyowekwa na serikali.

Kuhusu kufungwa kwa baadhi ya shule za binafsi kutokana na ukosefu wa fedha baada ya kufungwa kufuatia mamabukizi ya korona, Waziri Magoha amesema serikali itahakikisha kwamba wanafunzi waliokuwa wakisomea katika shule hizo wanapata nafasi katika shule za umma.

Amesema serikali ina mpango wa kutoa mkopo wa shilingi bilioni 7 kwa shule za binafsi ili kuziwezesha kurejelea shughuli zitakapofunguliwa mwakani.