array(0) { } Radio Maisha | Watu 599 wameambukziw akorona katika saa 24 zilizopita
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 599 wameambukziw akorona katika saa 24 zilizopita

Watu 599 wameambukziw akorona katika saa 24 zilizopita

Watu mia tano tisini na tisa wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini humu katika saa ishirini na nne zilizopita.

Idadi hii imetokana na vipimo elfu nne mia nne na ishirini.

Idadi hii sasa inafikisha idadi jumla ya walioambukizwa nchini kuwa elfu ishirini na sita mia nne thelathini na sita .

Mia tatu sabini na watatu ni wanaume huku mia mbili ishirini na sita wakiwa wanawake, ambapo Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaoambukizwa.

Wakati uo huo, Kenya leo imerekodi idadi ya juu zaidi ya watu ambao wamethibitishwa kupona katika saa ishirini na nne zilizopita, ambao ni watu elfu moja na sitini na wawili.

Idadi jumla ya waliopona sasa ni elfu kumi na mbili mia tisa sitini na mmoja.

Hata hivyo, watu wengine wawili wamefariki dunia na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kuwa mia nne na ishirini.

Hayo yakijiri,  Waziri Kagwe amewaonya madaktari hasa wa hospitali za binafsi wanaotoa vyeti vya watu ambao hufariki dunia kutokana na Ugonjwa wa COVID-19 ili kuonesha kwamba hawakuwa wameambukizwa.

Waziri Kagwe, amesema imebainika kwamba baadhi ya madaktari wamekuwa wakifanya hivyo ili kuiruhusu familia ya mwendazake kumzika, bila kufuata masharti ya kuwazika wanaofariki dunia kutokana na COVID-19 kwa lengo la kuepuka unyanyaopaa.

Amesema hatua hiyo inahatarisha maisha, kwani virusi hivyo vinaweza kusambaa hata mtu anapokuwa amefariki dunia.