array(0) { } Radio Maisha | Raila atakuwa rais 2022 -David Murathe
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila atakuwa rais 2022 -David Murathe

Raila atakuwa rais 2022 -David Murathe

Jiandaaeni kuongozwa na Raila Odinga baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, ndiyo kauli ya Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Jubilee David Murathe.

Akizungumza kwenye mahojiano ya kipee na Runinga ya KTN News , Murathe amesema umefika wakati sasa wa Wakenya kumtunuku kiti cha Urais Raila Odinga kutokana na juhudi zake za kuleta mabadiliko katika masuala mbalimbali yaliyochangia ukuaji wa taifa hili.

Akitoa mfano wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela jinsi alivyopigania taifa hilo na hatimaye kuwa rais, Murathe amesema yeye mwenyewe atampigia kura Raila Odinga kuwa Rais wa Taifa hili katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Aidha amemwomba Raila kuwa Rais wa muhula mmoja na aondoke ofisini kwa amani na kuwapisha wengine kuwania kiti hicho.

Kwa mujibu wa Murathe kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, kitakuwa na wagombea mbalimbali na kwamba atakuwapo mgombea wa mwafaka kati ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta yaani Handshake. Murathe amesema hakuna pinganimizi yoyote kwa Raila kuwa Rais wa taifa hili, na kwamba iwapo hatawania basi yeye na eneo la Mlima Kenya watakuwa tayari kumuunga mkono mgombea atakayependekezwa na Rais Kenyatta na Raila Odinga, ila kwa sasa ana uhakika kwamba ni wakati wa Raila kuliongoza taifa hili baada ya uchaguzi wa mwaka 2022.

Kauli ya Murathe inajiri siku moja tu baada ya Mbunge wa Cherangany Jushua Kutuny kudai kwamba kinyamgayiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 kitakuwa baina ya Naibu wa Rais William Ruto na Raila Odinga. Aidha alisema kuwa ushindani mkali utategemea na mgombea atakayeungwa mkono na Rais Kenyatta.