array(0) { } Radio Maisha | Mwili wa Marehemu, Kajembe umezikwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwili wa Marehemu, Kajembe umezikwa

Mwili wa Marehemu, Kajembe umezikwa

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Changamwe Ramadhan Kajembe umezikwa nyumbani kwake katika eneo la Kwa shee , Jomvu kwenye Kaunti ya Mombasa.

Waliohutubu ni mwanawe Sudi Kajembe na Mshirikishi wa Utawala kwenye eneo la Pwani John Elungata.

Shughuli ya mazishi imeongozwa na maafisa kumi wa afya na kufuatia utaratibu uliowekwa na wizara ya afya kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.

Mamia ya jamaa zake wamehudhuria hafla hiyo.

Marehemu Kajembe alifariki jana jioni katika hospitali ya Pandya mjini Mombasa. Kifo chake kimejiri wiki mbili tu baada ya kifo cha mkewe  wa kwanza Aziza Kajembe aliyekuwa akiugua ugonjwa wa Covid 19.

Kadhalika mwezi Machi mwaka huu, Kajembe alifiwa mke wake wa pili Zaharia Kajembe.

Ramadhan Seif Kajembe alihudumu kati ya mwaka 1997 na 2007 kabla ya wadhfa huo kutwaliwa na Omar Mwinyi.