array(0) { } Radio Maisha | Kalonzo abadili msimamo kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kalonzo abadili msimamo kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato

Kalonzo abadili msimamo kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato

Kinara wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka sasa amewahimiza maseneta kuzingatia katiba ya mwaka 2010 katika ugavi wa mapato inayohimiza kuwapo kwa usawa katika ugavi wa rasilimali.

Kwa mujibu wa Kalonzo, maseneta wanapaswa kukumbatia juhudi za Spika wa Seneti Ken Lusaka za kufanya mazungumzo ya jinsi ya kupata mwafaka wa mswada huo tata ambao mjadala wake umeahirishwa kwa mara ya saba sasa katika seneti.

Kinyume na msimamo wake wa awali, Kalonzo amesema usawa katika ugavi wa mapato ndio njia pekee itakayohakikisha kwamba taifa hili linasonga mbele kimaendeleo.

Wakati uo huo amesema pana haja ya mgao wa Hazina ya Equalization Fund unapaswa kuongezwa ili kuzisaidia kaunti nyingine ambazo zinakumbwa na changamoto ikiwamo ukame, zinapata fedha za ziada za kuendesha shughuli zao.

Kauli ya Kalonzo inajiri siku kadhaa tu baada ya Kinara wa ODM Raila Odinga naye kubadili msimamo wake kuhusu mswada huo tata ambao kufikia sasa, umeligawanya bunge la seneti katika makundi mawili.

Ikumbukwe Naibu wa Rais William Ruto alikuwa miongoni mwa vigogo wa kwanza kupendekeza kutumika kwa mfumo wa awali ili kuhakikisha kwamba kila kaunti inanufaika.

Ikumbukwe jana mkutano wa kutafuta mwafaka baina ya makundi hayo zilikosa kuzaa matunda baada ya maseneta wa upande wanaopinga mswada huo kukosa kutuma wawakilishi wao.

Kikao cha kujadili mswada huo kinatarajiwa kufanyika Jumanne wiki ijayo