array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya walioambukizwa virusi vya korona nchini imepita elfu ishirini na tano
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Idadi ya walioambukizwa virusi vya korona nchini imepita elfu ishirini na tano

Idadi ya walioambukizwa virusi vya korona nchini imepita elfu ishirini na tano

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya korona nchini sasa imepita elfu ishirini na tano.

Wizara ya Afya Ijumaa imethibitisha kuwa watu wengine mia saba ishirini na saba wameambukizwa virusi hivyo hatari vinavyosababisha Ugonjwa wa Covid-19 na kufikisha jumla ya watu elfu ishirini na tano, mia moja thelathini na wanane.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, Jumla ya sampuli elfu sita mia nane kumi na nne zimefanyiwa vipimo katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita ambapo watu wengine mia saba ishirini na saba wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona. Aidha, watu mia saba kumi na mmoja ni Wakenya huku kumi na sita wakiwa raia wa kigeni.

Kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika kwenye Kaunti ya Kisii, Kagwe aidha amesema Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa idadi ya juu ya maambukizi, akiwashauri Wakenya wanaoishi Nairobi kutosafiri nyumbani na iwapo pana lazima wazingatie masharti yaliyowekwa na serikali.

Vilevile, idadi ya watu wanaopona Ugonjwa wa Covid-19 imeendelea kuongezeka baada ya  watu wengine mia sita sabini na wanne wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Watu mia moja ishirini na watano miongoni mwa mia sita sabini na wanne waliopona walikuwa wakihudimiwa nyumbani huku wengine waliosalia wakiwa kwenye vituo mbalimbali vya waathiriwa wa virusi virusi vya korona.

Kwa jumla watu elfu kumi na moja, mia moja kumi na wanane wamepona tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini.

Hata hivyo, watu wengine kumi na wanne wamethibitishwa kufariki katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita kutokana na makali ya Ugonjwa wa Covid-19.