array(0) { } Radio Maisha | Miaka 22 tangu shambulio la kigaidi katika ubalozi wa Marekani, Nairobi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Miaka 22 tangu shambulio la kigaidi katika ubalozi wa Marekani, Nairobi

Miaka 22 tangu shambulio la kigaidi katika ubalozi wa Marekani, Nairobi

Na caren Papai,

NAIROBI, KENYA, Kumbuka Ijumaa hii ni miaka ishirini na miwili tangu kutekelezwa kwa shambulio la kigaidi katika ubalozi wa Marekani hapa jijini Nairobi ambapo zaidi ya watu mia mbili walifariki dunia, na wengine zaidi ya elfu nne kujeruhiwa.

Shambulio hilo ililopangwa na Kiongozi wa Al queda Marehemu Osama Bin Laden lilitekelezwa pia katika Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Ikumbukwe Osama Bin Laden alifariki dunia Mei mwaka 2011 katika oparesheni iliyoongozwa na jeshi la Marekani.

Wahukiwa wengine wa shambulio hilo kama vile Mohammed Odeh, Rashed Daoud, Khalfan Khamis, na Mohammed Ghailani walipatikana na hatia na wanatumikia kifungo gerezani.

Hata hivyo, miongoni mwa washukiwa ishirini na mmoja ni watatu tu ambao wako mafichoni hadi sasa.

Watatu hao ni Ayma AlZawahiri aliyechukua nafasi ya Osama baada ya kufariki dunia na Saif Al Adel na Abudullah Ahamed Abudullah.