×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mswada wa Ugavi wa Mapato, ipi njia sawa

Mswada wa Ugavi wa Mapato, ipi njia sawa

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Kamati maalum iliyobuniwa kutafuta suluhu kufuatia utata katika seneti kuhusu mswada wa ugavi wa mapato inaanza vikao vyake rasmi Ijumaa.

Kamati hiyo ilibuniwa Jumatano, baada ya Seneti kukosa kuafikiana kuhusu mfumo unaostahili kutumika katika ugavi wa fedha kwa serikali za kaunti.

Hayo yanajiri huku mvutano ukiwa umeibuka kuhusu anayestahili kuiongoza kamati yenyewe, baada ya baadhi ya Maseneti kupinga uteuzi wa Naibu Spika Profesa Margaret Kamar wakisema tayari ameonesha kuunga mkono mfumo unaopendekezwa na Tume ya Ugavi wa Mapato CRA.

Maseneta hao wanasema Kamar alishiriki kura Jumanne na kwamba kaunti yake ya Uasin Gishu ni miongoni mwa zitakazonufaika na mfumo huo wa CRA, huku wakipendekeza kamati hiyo iongozwe na Spika Ken Lusaka au Seneta wa Busia Amos Wako ambao hawakushiriki katika kura hiyo.

Tayari upande unaounga mkono mfumo wa CRA,  umewasilisha majina ya maseneta wanne kwenye kamati hiyo ambao ni Seneta wa Nyeri Iphrahim Maina, mwenzake wa Nandi Samson Cherargey, Seneta wa Nakuru Susan Kihika, Seneta wa Migori Ochilo Ayacko na Seneta Maalum Naomy Shiyonga.

Hata hivyo, upande unaopinga mfumo wa CRA ukiongozwa na seneta wa Nairobi Johnson Sakaja na mwenzake wa Makueni Mutula Kilonzo Jrn haujawasilisha orodha yake.

 

Ripoti ya kamati hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa viongozi wa vyama ya kisiasa, akiwamo Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wa Rais William Ruto na Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga.  Rais Kenyatta amesalia kimya hadi kufikia sasa huku Naibu wake akiwashauri maseneta kutafuta mwafaka kwani tayari mvutano huo umeleta mgawanyiko. Kwa upande wake Raila anapendekeza kwamba sharti kaunti zote zinufaike.

 

Maseneta watafanya kikao kisicho rasmi yaani Kamukunji Jumatatu ijayo, ambapo pande zote mbili zitatafuta uungwaji mkono, kabla ya vikao vya Jumanne ambapo kura itapigwa.