array(0) { } Radio Maisha | Jaji Mkuu aendeleza shutma dhidi ya Serikali Kuu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jaji Mkuu aendeleza shutma dhidi ya Serikali Kuu

Jaji Mkuu aendeleza shutma dhidi ya Serikali Kuu

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Jaji Mkuu David Maraga, ameendeleza shutma dhidi ya Serikali kufuatia mgao mdogo wa fedha kwa Idara ya Mahakamana akisema hatua hiyo inaathiri pakubwa shughuli zake.

Maraga ameonya kwamba iwapo Idara hiyo haitatengewa fedha za kutosha, basi mfumo wake wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia uliozinduliwa hivi maajuzi huenda ukasambaratika.

Jaji Mkuu amesema kuwa ukosefu wa fedha, umetatiza mfumu huo wa kuwasilisha kesi kijiditali uliolenga kupunguza mirundiko ya kesi mahakamani.

Maraga amesema kwamba mfumo huo unaendelea vyema isipokuwa changamoto kadhaa ambazo zinaendelea kushughulikiwa huku asilimia 67 ya wanaosaka huduma za idara hiyo, wakielezea kuridhishwa na utendakazi wake, kwa mujibu wa ripoti ya utafiti ya hivi karibuni.

Hii si mara ya kwanza kwa Maraga kulalamikia kutengwa kwa Idara ya Mahakama na serikali, suala ambalo limezidisha uhasama baina yake na Rais Uhuru Kenyatta hasa baada ya Rais Kukataa kuidhinisha uteuzi wa majaji 41.