×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wabunge waliostaafu kulipwa 100,000 kila mwezi

Wabunge waliostaafu kulipwa 100,000 kila mwezi

Wabunge waliohudumu kati ya mwaka 1984 na 2001 wataanza kulipwa shilingi laki moja kila mwezi, iwapo rais Uhuru Kenyatta atatia saini marekebisho katika sheria ya malipo ya kustaafu ambayo yameidhinishwa na Bunge la Kitaifa leo hii.
Marekebishoo hayo yaliyowasilishwa na Kiongozi wa Wachache katika Bunge hilo ohn Mbadi yanalenga kuwasaidia wabunge hao wa zamani ambapo wamekuwa wakilalamikia malipo duni wanayolipwa baada ya kustaafu.

Akitetea marekebisho yake wakati wa kikao cha bunge asubuhi, Mbadi amesema hatua hiyo haitaigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha hasa baada ya kuondoa pendekezo kwamba walistahili kuanza kulipwa kuanzia mwaka 2010.

Mbadi amesema sasa serikali itahitaji shilingi milioni mia moja arubaini na nne pekee kila mwaka wa kifedha kuwalipa wabunge hao ambao ni mia moja hamsini.

Aidha, Mwakilishi wa Kike wa kaunti ya Homa Bay Gladys Wanga, amesema kupitishwa kwa marekebisho hayo kutawasaidia pakubwa wabunge hao wa awali.

Kauli ya Wanga imeungwa mkono na Kiongozi wa Wengi Amos Kimunya.

Wabunge wengi wameunga mkono marekebisho hayo huku wakimwomba rais uhuru Kenyatta kutia saini.

Hata hivyo, aliyekuwa Kiongozi wa Wengi ambaye pia ni Mbunge wa Garissa Mjini Adan Duale amekuwa na hisia tofauti akisema huenda baadhi ya wafanyakazi katika sekta za umma pia wakafuata mkondo huo kutaka malipo yao ya kustaafu yaongezwe.

Katika kikao cha alasiri Wabunge hoja iliyowasilishwa na Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime akipendekeza Wabunge ambao wamehudumu kwa muhula mmoja kulipwa malipo ya uzeeni

Kwa sasa wabunge ambao wamehudumu mihula miwili au zaidi ndio pekee wanastahili pokea malipo hayo.

Hayo yamejiri huku Wakenya wengi wakiwamo viongozi wa kidini wakikashifu hatua ya wabunge kupitisha mswada huo wa kuongeza marupurupu kwa wabunge waliostaafu

Abubakar Bini ni Mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Dini ya Kiislamu.

Bini anasema badala ya wabunge waliostaafu kuongezewa marupurupu, serikali inafaa kuweka mikakati zaidi ya kuwaajiri mamilioni ya vijana wasiokuwa na ajira.