array(0) { } Radio Maisha | Mjadala kuhusu mfumo mpya wa ugavi wa mapato waahirishwa kwa saba sasa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mjadala kuhusu mfumo mpya wa ugavi wa mapato waahirishwa kwa saba sasa

Mjadala kuhusu mfumo mpya wa ugavi wa mapato waahirishwa kwa saba sasa

Kwa mara ya saba sasa maseneta wamepoga kuairisha mswada tata wa mfumo mpya wa ugavi wa mapato kwenye serikali za kaunti.

Maseneta 34 dhidi ya 26 wamepiga kura kuahirisha kujadiliwa kwa mswada huo huku Seneta wa Busia Amos Wako akiwa wa pekee aliyekosa kupiga licha ya kuhushuria kikao cha leo.

Mswada huo uliwasilishwa na Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen akiwashauri masneta kuunga mkono ili kutoa nafasi zaidi ya maseneta kujadiliana kuhusu mapendekezo ya mswada huo tata.

Akiwasilisha hoja hiyo, Murkomen amesema Wakenya wanaendelea kutaabika na kwamba pana haja ya seneti kuahirisha kikao hicho na kufanya mkutano wa dharura wa jinsi ya kusaka mwafaka wa kuhakikisha kitita cha shilingi bilioni 316.5 kitakavyosambazwa kwenye serikali za kaunti.

Murkomen amesema maseneta wanapaswa kuwa mustari wa mbele kuwaunganisha Wakenya kwa kuhakikisha kila kaunti inapata fedha inazostahili ili kuwahudumia Wakenya mashinani.

Seneta wa Vihiga George Khaniri ameunga mkono kuahirishwa kwa kikao hicho akisema maseneta sasa wana muda mwafaka wa kuyatathmini mapendekezo ya mswadam huo, kisha kubaini jinsi ya kuhakikisha kwamba fedha hizo zinagawanywa kwa usawa

Aidha Seneta wa Kiambu Kimani Wamatangi amepinga hatua ya kuahirishwa kwa kikao hicho akisema haitasaidia kutatua changamoto zinazowakumba Wakenya mashinani.

Wamatangi amesisistiza kwamba Kaunti hazina fedha za kuendesha huduma mashinani.

Katika kikao hicho nusura Kiranja wa Wengi Irungu Kang'ata akosane na Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja baada ya Sakaja kudai kwamba maisha yake yako hatarini kufuatia msimamo wake kuhusu mswada huo, Kang'ata akisisitiza kwamba amekuwa akiyatekeleza majukumu yake ipasavyo likiwamo la kuwahakikishia maseneta ulinzi wa kutosha.

Akichangia baada ya kuahirishwa kwa mswada huo, Kiongozi wa Wachache James Orengo ameiomba seneti kutoa muda wa kutosha na hata kupendekeza jumanne wiki ijayo kwa mashauriano kufanyika kabla ya kuwasilishwa na kujadiliwa bungeni.

Imemlazimu Seneta wa Bungoma Moses Wetangula kunukuu baadhi ya vifungu vya vitabu vya tamthilia ili kuhakikisha kwamba pendekezo lake la awali la kutaka muda zaidi kwa mswada huo kujadiliwa linaeleweka.

Hata hivyo, kinyume na kawaida, Kiongozi wa Wengi wa Seneti Profesa Samuel Poghisio amempongeza Murkomen kwa mswada huo, akisema sasa itawalazimu kushauriana kwa kina jinsi ya kufanikisha mswada huo.

Maseneta sasa wataibini Jumanne wiki ijayo mahali watakapofanya mkutano wa mashauriano kuhusu jinsi ya kuushughulikia mswada huo.