×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Bunge la Kaunti ya Nairobi lapendekeza Kitengo cha Huduma za Jiji NMS, kuendeleza miradi iliyokwama kwenye Wizara ambazo zilihamishwa kwa serikali kuu

Bunge la Kaunti ya Nairobi lapendekeza Kitengo cha Huduma za Jiji NMS, kuendeleza miradi iliyokwama kwenye Wizara ambazo zilihamishwa kwa serikali kuu

Bunge la Kaunti ya Nairobi sasa linapendekeza Kitengo cha Huduma za Jiji Nairobi Metropolitan Services NMS, kuendeleza miradi iliyokwama kwenye Wizara ambazo zilihamishwa kwa usimamizi wa Serikali ya Kitaifa.

Wawakilishi Wadi wameilaumu serikali ya kaunti kwa kushindwa kutekeleza miradi chini ya Wizara hizo wakisema mvutano unaoendelea baina ya Gavana Mike Sonko na Mkurugenzi Mkuu wa NMS Jenerali Mohamed Badi umesababisha hali hiyo.

Kupitia hoja iliyowasilishwa bungeni na Mwakilishi Wadi ya Clay City Samora Mwaura, wawakiishi hao wameitaka NMS kushughulikia miradi yote iliyokwama.

Mzozo umekuwa ukiendelea baina ya Gavana Mike Sonko, Jenerali badi na Spika Beatrice Elachi kuhusu suala la uongozi na madai ya kuhujumu utendakazi, Sonko akimsuta Badi kwa kupiga vita mikakati yake ya maendeleo.

Sonko tayari ameanzisha mchakato wa kuerejesha majukumu aliyotia saini kuhamishwa kwa Serikali Kuu akisema kuwa maafikiano kuhusu mkataba huo yamekiukwa.