array(0) { } Radio Maisha | Baadhi ya maseneta wasimama kidete
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Baadhi ya maseneta wasimama kidete

Baadhi ya maseneta wasimama kidete

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Kinachoendelea katika Bunge la Seneti kuhusu Mswada tata wa Ugavi wa Mapato ni ishara tosha ya kuendelea kukomaa kwa demokrasia nchini.

Baadhi ya Maseneta akiwamo wa Makueni Mutula Kilonzo Jr, wamenakiliwa na vyombo vya habari wakisema kwamba wanaendelea kushinikizwa na viongozi wa vyama vyao vya kisiasa kuupitisha mswada huo japo wamesimama kidete kutetea wanachohisi kuwa ni sawa kwa taifa hili na wananchi kwa jumla.

Bila shaka ni ujumbe tosha kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga kwamba ni mwamko mpya katika masuala yanayowahusu wananchi na pengine changamoto kwa Wabunge kuendeleza mkondo wa kusimamia haki badala ya kushawishiwa na vyama kuegemea upande mmoja jinsi imekuwa ikishuhudiwa bungeni mara kwa mara.

Radio Maisha imebaini kwamba maseneta 25 waliochangia kuangushwa kwa hoja iliowasilishwa na Seneta wa Murang'a Irungu Kang'ata, vilevile wamepanga kufanya hivyo wakati wa kikao cha leo, huku wakielezea wazi sababu zao.

Iwapo idadi hiyo ya maseneta wanaoupinga mswada huo itasalia 25, watakuwa wamezidi idadi ya maseneta 24 wanaohitajika kuuangusha mswada huo , ambao iwapo utapitishwa utazipokonya kaunti 18 nchini kima cha shilingi bilioni 17.

Jumapili wiki iliyopita, Raila alikutana na baadhi ya wandani wa Rais Uhuru akiwamo Naibu Mwenyekiti wa Jubilee David Murathe nyumbani kwa Katibu Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi, COTU Francis Atwoli ambako inaaminika suala hilo lilijadiliwa kwa kina.