array(0) { } Radio Maisha | Seneti kupiga kura kuhusu mswada wa ugavi wa mapato
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Seneti kupiga kura kuhusu mswada wa ugavi wa mapato

Seneti kupiga kura kuhusu mswada wa ugavi wa mapato

Na Caren Papai,

NAIROBI, KENYA, Macho yote Jumanne hii yanaelekezwa katika Bunge la Seneti kuona iwapo Maseneta wataafikiana kuhusu mvutano unaozingira Mswada tata wa ugavi wa mapato kwa kaunti.

Chama cha Jubilee tayari kimewaonya vikali Maseneta waasi ambao walipinga pendekezo la Kiranja wa Wengi Irungu Kang'ata wiki iliyopita kuhusu mfumo wa kuzingatia idadi ya watu kwa kaunti.

Naibu Mwenyekiti wa Jubilee David Murathe amewaonya Maseneta saba wakiwamo Johnson Sakaja, Kipchumba Murkomen na Anwar Loitiptip ambao wanaendeleza vugu vugu kwa jina ''One Kenya Movement'' wakilenga kuhakikisha kuwa hakuna kaunti inapoteza mgao wa fedha.

Maseneta Jumanne watajadali ripoti ya Kamati ya Fedha inayoungwa mkono na Tume ya Ugavi wa Mapato CRA , ambapo iwapo itapitishwa basi fedha za kaunti 18 zitapungwa huku Kaunti 29 zikipewa mgao mnono wa fedha.

Aidha, Seneti itajadili mapendekezo ya Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja anayeshinikiza mfumo wa sasa  ufanyiwe marekebisho na kutumika kusambaza fedha kwa kaunti kuhakikisha kuwa kila kaunti inapewa mgao unaostahili.

Vilevile, Maseneta Mutula Kilonzo Jnr na Cleophas Malala miongoni mwa wengine,  wanapania kuwasilisha mapendekezo mapya yanayounga mkono yale ya Sakaja.  Mutula amesema kuwa hatakubali baadhi ya kaunti kunufaika na nyingine kutengwa.

Murathe ambaye awali alifanya kikao na  Kinara wa ODM Raila Odinga,  amewashauri Maseneta kupitisha mapendekezo ya CRA kuhusu mfumo unaopigawa upatu wa idadi ya watu kwa kaunti.

Haya yanajiri huku Magavana wakishindwa kuafikiana na Hazina ya Kitaifa na Tume ya Ugavi wa Mapato kuhusu shilingi bilioni 29 za bajeti ya mwaka wa kifedha uliopita.

CRA imesema i tayari kuidhinisha asimilia 50 ya fedha hizo kwa kaunti iwapo mzozo wa ugavi wa mapato hautapata suluhu, suala linalopingwa na Magavana wanaosema huduma kwa kaunti zinataendelea kutatizika.