array(0) { } Radio Maisha | Watu 13 waaga dunia na 544 kuambukizwa.
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 13 waaga dunia na 544 kuambukizwa.

Watu 13 waaga dunia na 544 kuambukizwa.

Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja ni miongoni mwa watu 544 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini leo hii.

Katika taarifa yake ya takwimu za maambukizi, Wizara ya Afya imesema kuwa watu hao wamethibitishwa baada ya sampuli elfu mbili mia sita hamini na tatu katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Aidha Wizara ya Afya imesema miongoni mwa walioambukizwa, mia nne arubaini na tisa ni Wakenya huku arubaini na watano wakiwa raia wa mataifa ya kigeni.

Kwa jumla Kenya sasa ina visa elfu ishirini na mbili, mia tano tisini na saba vya korona baada ya sampuli elfu mia tatu kumi na nane, mia tatu sabini na sita kufanyiwa vipimo tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa.

Akihutubu muda muchache uliopita, Katibu wa Utawala wa Wizara ya Afya Daktari Rashid Aman amesema watu wengine mia mbili sitini na watatu wamepona, ambapo mia moja sabini na sita walikuwa wakitibiwa nyumbani huku waliosalia wakipona kwenye hospitali mbalimbali na kufikisha watu elfu nane mia saba arubaini, jumla ya waliopona.

<AUDIO>5022

Aidha katika takwimu hizo, kaunti ya Nairobi imeendelea kuathiriwa zaidi na maambukizi ya korona vilevile kaunti ya Kiambu, Nakuru na Machakos, huku visa vya maambukizi kwenye kaunti za Mombasa na Kilifi vikiendelea kupungua kulinganishwa na awali.

Hata hivyo watu wengine kumi na watatu miongoni mwao mhudumu wa afya wa umri wa miaka thelathini na miwili wameaga dunia kutokana na makali ya Covid-19. Kumi miongoni mwao walikuwa wakiugua magonjwa sugu. Kwa jumla wahudumu wa afya wanane wamefariki kutokana na ugonjwa huo nchini.