array(0) { } Radio Maisha | Pendekezo la Sakaja kujadiliwa Jumanne kwenye Seneti
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Pendekezo la Sakaja kujadiliwa Jumanne kwenye Seneti

Pendekezo la Sakaja kujadiliwa Jumanne kwenye Seneti

Na Caren Papai,

Nairobi, Kenya, Kivumbi kinatarajiwa Jumanne katika Bunge la Seneti wakati wa kujadiliwa kwa mapendekezo ya Seneta wa Nairobi Johnston Sakaja ambaye anapendekeza mgao wa kaunti uzingatie mfumo wa sasa ili kuzuia kaunti kupoteza fedha za maendeleo.

Seneti iliahirisha vikao vya kujadili mswada tata wa ugavi wa mapato kwa Kaunti Jumanne wiki iliyopita kwa mara ya sita  ikiwa siku maalumu ya kujadili kwa hoja ya Sakaja, baada ya hoja ya Kiranja wa Seneti Irungu Kang'ata kuangushwa na maseneta.

Kang'ata alitaka mfumo mpya unaopendekeza idadi ya watu kuzingatiwa uanze kutumika baada ya miaka mitatu. Tayari Maseneta watatu wa eneo la Ukambani wamesisitiza kuwa hawatakubali kutishwa na yeyote au msukumo wa vyama kubadili msimamo wao kuhusu mswada huo.

Kwa mujibu wa Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Jnr, kuanzia wakati wa kuwasilishwa kwa hoja hiyo katika bunge la seneti, maseneta  wamekuwa wakishurutishwa na watu mbalimbali kuupigia debe mfumo mpya unaozingatia idadi ya watu kwa kaunti.

Kwa upande wake, Seneta wa Kitui Enock Wambua amesisita kuwa hakuna mapendekezo yamewasilishwa na Tume ya Ugavi wa Mapato CRA katika Bunge la Seneti na kuwa hoja iliyoko iliwasilishwa na Kamati ya Fedha.

Kauli za wawili hao imetiliwa mkazo na Seneta wa Machakos Boniface Kabaka , ambaye amesema kuwa maseneta hawatakubali maeneo fulani kunyanyaswa na mfumo huo mpya na mengine kupendelewa.

Kauli yao inajiri huku viongozi wa vyama vya ODM na Jubilee wakipanga kukutana leo na maseneta wa vyama vyao kuwashawishi kupitisha mswada huo hapo kesho.