array(0) { } Radio Maisha | Yatani kuongoza kikao kuhusu mswada wa ugavi wa mapato
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Yatani kuongoza kikao kuhusu mswada wa ugavi wa mapato

Yatani kuongoza kikao kuhusu mswada wa ugavi wa mapato

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Waziri wa Fedha Ukur Yattani anatarajiwa kufanya kikao Jumatatu asubuhi cha kutafuta mwafaka kuhusu mfumo mpya wa ugavi wa fedha kwa Serikali za Kaunti katika Bunge la Seneti, kabla ya kujadiliwa mara ya saba katika bunge hilo siku ya Jumanne.

Kikao hicho kinatarajiwa kuhudhuriwa na washikadau mbalimbali kujadili suala hilo, ambalo limeibua migawanyiko miongoni mwa maseneta huku viongozi wa mirengo ya Jubilee na ODM wakisalia katika njia panda baada ya kushindwa kuwashawishi maseneta wa mirengo yao kuunga mkono mfumo huo.

Siku ya Jumanne iliyopita wakati wa vikao vya kujadili mfumo huo bungeni, Kiongozi wa Wachache katika Seneti James Orengo alisema hali ya Rais Kenyatta kuwa mgumu wa kushauriana na viongozi wengine kuhusu mfumo huo ndiyo inatatiza kuidhiniswa kwake.

Aidha, ni Jumapili ambapo mwenyekiti wa ODM John Mbadi alisema mgogoro unaozuia kupitishwa kwa mfumo huo haufai kuhusishwa na ODM wala mpango wa Upatanishi BBI.

Kwa mujibu wa Mbadi, ODM haijatoa msimamo rasmi kuhusu mfumo huo unaopingwa na wengi kwa kupendekeza mgao wa fedha kutolewa kwa kuzingatia idadi ya watu katika kila kaunti ,badala ya ukubwa wa maeneo jinsi ilivyo sasa.