array(0) { } Radio Maisha | Muunguzi mwingine aaga dunia kutokana na Covid-19
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Muunguzi mwingine aaga dunia kutokana na Covid-19

Muunguzi mwingine aaga dunia kutokana na Covid-19

Na Caren Papai,

NAIROBI, KENYA, Kwa mara nyingine, sekta ya afya imepata pigo baada ya muuguzi mwengine kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Marian Awuor Adumbo ambaye alikuwa mhudumu wa Hospitali ya Karachuonyo alifariki dunia mapema Jumapili kufuatia matatizo ya kupumua yaliyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 baada ya kujifungua wiki moja iliyopita.

Marian mwenye umri wa miaka 32 alithibitishwa kuambukizwa virusi vya Korona tarehe 20 mwezi uliopita ,kisha kuwekwa katika oksijeni. Alijifungua tarehe 24 kisha mtoto kuwekwa katika mashine ya kumsaidia kukomaa yaani incubator.

Mumewe ambaye alizungumza na mwanahabari wetu wa masuala ya fya siku ya Jumamosi, siku moja tu kabla ya kifo cha mkewe alieleza matumaini  ya kumpeleka mkewe nyumbani kwani, alikuwa tayari amepona virusi hivyo baada ya kupimwa mara mbili.

Katika mahojiano ya simu, mumewe alieleza kuwa, Marian alitarajiwa kuanza kumyonyesha mwanawe kuanzia leo, asijue kuwa hata mkewe hataiona siku ya leo.

Mariano ni miongoni mwa wahudumu wa afya akiwamo  Dakta Doreen Lugaliki aliyefariki dunia mwezi uliopita na kuzikwa katika Kaunti ya Bugoma kutokana na Covid-19 huku wengine zaidi ya mia nne wakiambukizwa virusi vya korona.