array(0) { } Radio Maisha | Watu 690 zaidi wameambukizwa korona Kenya; 5 wameaga dunia
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 690 zaidi wameambukizwa korona Kenya; 5 wameaga dunia

Watu 690 zaidi wameambukizwa korona Kenya; 5 wameaga dunia

Watu mia sita tisini wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini katika saa ishirini na nne zilizopita. Idadi hii imetokana na sampuli elfu tano mia tatu tisini na tatu zilizopimwa katika sa aishirini na nne zilizopta.

Idadi jumla ya maambukizi nchini sasa ni elfu ishirini na mbili na hamsini na tatu.

Kuanti ya Nairobi imerekodi visa mia tano thelathini na vitano, Kiambu, hamsini na sita, Kaunti ya Kajiado ishirini na vinane, Nyeri ishirini na vinne, Busia tisa, Machakos  saba,Kisunu na Nakuru zote zina visa sita. Embu na Garissa zote zimerekodi visa vinne laikipia na Narok  vitatu huku kaunti za Bungoma, Kwale, Meru, Mombosa  na Nyandarua zikirekodi kisa kimoja kimoja.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba watu wengine hamsini na wanane wamethibitishwa kupona na kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa elfu nane mia nne sabini na saba.

Hata hivyo, idadi ya waliofariki dunia imefikia mia tatu sitini na tisa baada ya watu wengine watano wamefariki dunia katika saa ishirini na nne zilizopita.