array(0) { } Radio Maisha | Akombe; Chiloba alinionya dhidi ya kutoa ushahidi kufuatia kifo cha Msando
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Akombe; Chiloba alinionya dhidi ya kutoa ushahidi kufuatia kifo cha Msando

Akombe; Chiloba alinionya dhidi ya kutoa ushahidi kufuatia kifo cha Msando

Aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Uchaguzi IEBC Roselyn Akombe sasa anadai kwamba aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo Ezra Chiloba amemwonya dhidi ya kutoa ushahidi kuhusu kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa IEBC Chriss Musando.

Katika taarifa yake kwenye mtandao wa Twitter, Akombe ameuweka wazi ujumbe wa Chiloba mtandaoni ambapo ameambiwa asithubutu kuongea chochote kuhusu yaliyotukia hadi kifo cha Musando, Chiloba akisema kuwa kunyamaza kwao si idhini ya Akombe kutoa siri hiyo.

Ikumbukwe Julai 29, mwaka huu Akombe alisema kwamba mauaji ya Chris Msando yalisababishwa na watu fulani ndani ya IEBC akisema yu tayari kutoa ushahidi iwapo atatakiwa kufanya hivyo huku akiongezea kwamba wakuu serikalini hawajatilia maanani wito wakukamatwa kwa washukiwa huku akiishutumu Ofisi ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma kwa kuzembea kuhusu kesi hiyo.

Ikumbukwe mwili wa Musando ulipatikana katika kichaka kimoja kwenye Msitu wa Muguga, eneo la Kikuyu, mauaji ambayo nusra yatatize uchaguzi mkuu wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka 2017.

Uchunguzi wa awali ulibainisha kwamba marehemu aliteswa kabla ya kuuliwa huku mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwa kamba.