array(0) { } Radio Maisha | ''Hakuna kisa cha korona Samburu'' imesema Wizara ya Afya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

''Hakuna kisa cha korona Samburu'' imesema Wizara ya Afya

''Hakuna kisa cha korona Samburu'' imesema Wizara ya Afya

Wizara ya Afya imekana kuwa kuna kisa cha maambukizi ya virusi vya korona kwenye Kaunti ya Samburu kinyume na taarifa za awali.

Kaimu Mkurugenzi wa Matibabu katika Wizara hiyo Daktari patrick Amoth amesema kisa kilichoriportiwa ni kuhusu afisa wa polisi wa kaunti ya Samburu na kwamba maafisa wa afya wamewasilisna naye.

Mwathiriwa huyo amesema kwamba alifanyiwa vipimo kweney Kuanti ya Isiolo Ijumaa iliyopita na kupatikana kuwa ameambukizwa.

Haya yanajiri saaa chache tu baada ya Serikali ya Kaunti hiyo ya Samburu sasa kudai kuwa Wizara ya Afya inapotosha kuhusu maambukizi ya virusi vya korona ikisema hakuna kisa kilichoripotiwa.

Akizungumza kwenye Hopsitali ya Rufaa ya Maralal Gavana Moses  Lenolkul ameitaka Wizara ya Afya kuwa makini inapotoa takwimu kuhusu mamabukizi nchini.

Amesema serikali yake imeimarisha miakakati kuhakikisha kwamba hakuna maambukizi yanaripotiwa kwenye kaunti hiyo.

Aidha amesema amenunua magari matatu ya ambulensi yatakayowashughulia wagonjwa wa COVID-19, akisema tangu mwezi machi ni sampuli kati ya mia mbili na mia tatu zilizotumwa katika maabara jijini Nairobi kufanyiwa vipimo, kwani hakuna kituo cha kupima korona kwenye kaunti hiyo.

Hapo jana wakati wa kutoa takwimu za kila siku Waziri Mutahi Kagwe alitangaza kuwa kisa cha kwanza kimeripotiwa kweney kaunti ya Samburu hivyo kaunti zote arubaini na saba zimeathirika