array(0) { } Radio Maisha | ODM imejitenga na mvutano kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato katika seneti
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

ODM imejitenga na mvutano kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato katika seneti

ODM imejitenga na mvutano kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato katika seneti

Mwenyekiti wa Chama cha ODM John Mbadi amesema mgogoro unaozuia kupitishwa kwa mfumo mpya wa ugavi wa fedha za kaunti katika Bunge la Seneti haufai kuhusishwa na ODM wala mpango wa Upatanishi BBI.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Runinga ya KTN NEWS, Mbadi ambaye pia ni Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa amesema tofauti inayoshuhudiwa miongoni mwa maseneta inatokana na majukumu yao ya kutetea kaunti wanazowakilisha bungeni.

Mbadi amesema ODM haijatoa msimamo wowote rasmi kuhusu mfumo huo unaopingwa na wengi kwa kupendekeza mgao wa fedha kutolewa kwa kuzingatia idadi ya watu katika kila kaunti.

Kuhusu hatua ya baadhi ya wabunge wa eneo la Pwani akiwamo Aisha Jumwa wa Malindi na Mohammed Ali wa Nyali kusema ODM imewasaliti Wapwani kwa kufeli kuwatetea, Mbadi amesema wabunge walioongea ni wa mrengo wa Naibu wa Rais Wiliam Ruto ambao wanalenga kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Kauli ya Mbadi ambaye ni mshirika wa Raila Odinga imejiri baada ya madai kusambaa kwamba hali ya mfumo huo kufeli kupitishwa mara sita katika seneti imetokana na migawanyiko baina ya mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta na Raila kuhusu jinsi ya kuangazia mfumo huo bila kuathiri maeneo yenye ufuasi mkubwa wa ODM.

Siku ya Jumanne iliyopita wakati wa vikao vya kujadili mfumo huo bungeni, Kiongozi wa Wachache katika Seneti James Orengo alisema hali ya Rais Kenyatta kuwa mgumu wa kushauriana na viongozi wengine kuhusu mfumo huo ndiyo inayoathiri kuidhiniswa kwake.

Tayari Waziri wa Fedha Ukur Yattani ameitisha kikao kesho ili kutafuta mwafaka kuhusu mfumo huo ambao unatishia kuathiri huduma za serikali za kaunti kabla ya kuadiliwa mara ya saba katika bunge la seneti siku ya Jumanne ijayo.