array(0) { } Radio Maisha | Kenya imekana kupiga marufuku ndege kutoka baadhi ya mataifa dhidi ya kuingia nchini
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya imekana kupiga marufuku ndege kutoka baadhi ya mataifa dhidi ya kuingia nchini

Kenya imekana kupiga marufuku ndege kutoka baadhi ya mataifa dhidi ya kuingia nchini

Serikali imekana madai kuwa imepiga marufuku ndege kutoka baadhi ya mataifa dhidi ya kuingia ncchini.

Waziri wa Uchukuzi James Macharia amefafanua kwamba mataifa ambayo ndege zao zimeruhusiwa kusafiri kuja humu nchini ni yale yaliyoafikia masharti ya kudhibiti amabukizi ya virusi vya korona.

Waziri Macharia amesema amefanya mazungumzo na mwenzake wa Tanzania kuhusu hatua ya kupiga marufuku shirika la Ndege la Kenya Airways dhidi ya kusafiri kuelekea nchini humo.

Waziri Macharia amesema Kenya inatarajia kwamba kabla ya mwisho wa siku ya leo, Tanzania itabadilisha hatua hiyo akisisitiza kwamba hakuna mzozo wowote wa kidiplomasia baina ya mataifa haya mawili.

Macharia ameendelea kuitetea hatua ya serikali kutolijumuisha taifa la Tanzania kwenye orodha ya mataifa ambayo ndege zake zitaruhusiwa kuingia humu nchini, akisema kuna utaratibu wa afya unaostahili kufuatwa ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.

Leo hii safari za ndege za kimataifa zimerejelewa zaidi ya miezi minne tangu zilipositishwa kufuatia maambukizi hayo, huku Waziri Macharia akisema tayari mashirika kadhaa ya ndege yameanza rasmi safari hizo punde tu baada ya anga za Kenya kufunguliwa.

Ndege nne zimeondoka mapema leo kuelekea Uingereza, Dubai, Addis Ababa nchini Ethiopia na Dakar nchini Senegali.

Aidha, Ndege tatu zinatarajiwa kuwasili leo jioni nchini humu, ambazo mbili zinatoka Uingereza na moja kutoka Ujerumani.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kuruhusiwa kwa ndege za kimataifa kuingia ncini humu, hakumaanishi kwamba visa vya maaabukizi vimepungua bali ni jukumu la serikali kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida, huku akiwashauri

Kuhusu jindi Kenya ilivyoafikia orodha ya mataifa ambayo ndege zake zitaruhusiwa kuingia nchini  Kaimu Mkurugenzi wa Matibabu wa Wizara ya Afya, Daktari Patrick Amoth, amesema kwamba serikali iliyaweka mataifa katika makundi matatu kuambatana na maambukizi ya korona.