×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hakuna mzozo wa kidiplomasia baina ya Kenya na Tanzania -Serikali

Hakuna mzozo wa kidiplomasia baina ya Kenya na Tanzania -Serikali

Hakuna mzozo wa Kidipolomasia baina ya Kenya  na Tanzania; amesema Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje Ababu Namwamba. Akizungumzia hatua ya wajumbe waliotumwa kumwakilisha Rais Uhuru Kenyatta wakati wa hafla ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Benjamin Mukapa, kurejea hata kabla ya kuwasili, Ababu amesisitiza kwamba kulikuwapo tu na hitilafu katika ndege waliyokuwa wakitumia.

Katibu huyo mkuu amesema Kenya itaendelea kushirikiana na Tanzania akisema mataifa haya yamekuwa marafiki kwa muda mrefu, akisema Rais Kenyatta na Magufuli wataendelea kushirikiana kwa manufaa ya Mataifa ya Afrika Mashariki.

Alikuwa akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua rasmi safari za kimataifa za ndge katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa JKIA ambayo imefanyika mapema leo.

Ngede ya kwanza ambayo imeondoka nchini ni ile ya moja kwa moja kuelekea London Uingereza huku Namwamba akisema ushirikiano wa Kenya na taifa hilo ni muhimu hasa kibiashara.

Katibu wa Wizara ya Uchukuzi Solomon Kitungu amesema kuwa kila baada ya miezi mitatu serikali itakuwa ikitathimini mikakati yake kuhakikisha virusi vya korona vinadhibiyiwa.

Wakati uo huo, Shirika la Ndege la Kenya Airways limeelezea kufurahishwa kwake na kurejelewa kwa safari hizo, likisema litahakikisha kuwa wasafiri wanaotumia ndege za shirika hizo wako salama.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika hili Alllan Kilavuka amesema kuwa Shirika hilo lilikuwa limeathirika pakubwa na usitishwaji wa safari hizo hivyo wana imani kuwa hali itaimarika hasa kwa wafanyakazi wake.

Ikumbukwe Kenya imeyaidhinisha mataifa kumi na saba ambayo ndege zake zitaruhusiwa kuingia nchini.  Matiafa hayo Korea Kusini, Uchina, Japan, Canada, Uswizi, Rwanda, Uganda, Namibia, Morocco vilevile Zambabwe.

Mataifa mengine ni Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Qatar vilevile Italia. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya orodha hiyo hata hivyo itakuwa inatathiminiwa kila siku ambapo mataifa mengine yataongezwa au kuondolewa.