×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Ken Ouko ameaga dunia

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Ken Ouko ameaga dunia

Mwanasosholojia vilevile Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi Ken Ouko ameaga dunia. Ouko ameaga dunia leo asubuhi baada ya kuugua ugonjwa wa Covid-19.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Nairobi John Orindi ambaye amesema Ouko ameaga dunia akiwa hospitalini akitibiwa.

Wakenya wanaendelea kumwomboleza Ken Ouko kwenye mtandao wa twitter. Miongoni mwa waliomwomboleza ni aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Muungano wa NASA Norman Magaya ambaye amesema Ouko alifanya somo la Ssholojia kuwa rahisi kwa wanafunzi wake na kwamba ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa.

Vilevile aliyekuwa mgombea wa Chama kiti cha Ubunge wa Kibra wa cha ANC Eliud Owalo amemwomboleza Ken Ouko akisema kuwa alikuwa rafikiye wa karibu. Amemkumbuka hasa wakati walipokuwa katika Chuo Kikuu cha Maseno jinsi alivyokuwa akimsaidia kimawazo.