×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya imerekodi idadi ya juu zaidi ya mamabukizi -watu 960

Kenya imerekodi idadi ya juu zaidi ya mamabukizi -watu 960

Kenya leo imerekodi idadi ya juu zaidi ya watu walioambukizwa virusi vya korona katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita, ambapo watu mia tisa sitini wameripotiwa kuambukizwa .

Idadi hii ni kutokana na sampuli elfu nane mia mbili sitini na moja zilizopimwa katika kipindi hicho.

Jumla ya watu walioambukizwa Korona nchini humu sasa ni elfu kumi na saba, mia sita na watatu

Miongoni mwa visa vipya mia tisa na sitini vilivyoripotiwa na Wizara ya Afya, Nairobi imeendelea kuongoza kwa maambukizi ambapo leo hii imerekodi visa mia tano na kumi, ikifuatwa na Kajiado yenye visa mia moja na viwili, Kiambu mia moja, , Makueni hamsini na vinane, Mombasa arubaini na vinane,  Busia ishirini na kimoja, Kajiado kumi na saba, Kisumu kumi na vinne na Nakuru kumi na viwili.

Aidha, wagonjwa mia moja sitini na tisa wa COVID-19 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani, hivyo kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa  elfu saba, mia saba na arubaini na watatu.

Hata hivyo, wagonjwa wawili wameaga dunia na kuongeza idadi ya waliofariki nchini humu kutokana na Korona kuwa mia mbili na themanini.