×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wanaougua magonjwa mengine wanazidi kufariki msimu huu korona

Wanaougua magonjwa mengine wanazidi kufariki msimu huu korona

Wizara ya Afya imeripoti idadi kubwa ya watu wanaougua magonjwa mengi yakiwamo Kisukari, tatizo la damu na ukimwi wakiendelea kufariki dunia wakati huu wa maambukizi ya korona.

Wizara ya Afya imetolea mfano ugonjwa wa Ukimwi, ambapo asilimia 96 ya waathiriwa wako katika matibabu ya kuzuia makali ya virusi vya HIV na hivyo basi wanastahili kuendelea kupokea matibabu pasi na uonga wa kutembelea vituo vya afya.

Akizungumza wakati wa kutoa takwimu za maambukizi ya kila siku, Katibu wa Utawala katika Wizara ya Afya Dakta Mercy Mwangangi amesema kuwa asilimia 90 ya wagonjwa hao wa Ukimwi wamefanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Mwangangi hata hivyo, amepongeza juhudi za kukabili janga la ukimwi nchini akisema kuwa maambukizi yamepungua kutoka visa 100,000  vya mwaka wa 2012 hadi visa 36,000 katika mwaka wa 2018. Aidha amesema kuwa Kenya kufikia sasa imetoa dawa za kukabili makali ya virusi hivyo ARV's kwa watu milioni 1.1.

Wakati uo huo, Wizara ya Afya imelalamikia hatua ya wagonjwa wa Ukimwi kuogopa kuviotembelea vituo vya afya kupokea matibabu huku Idadi kubwa ya Wakenya wakiohofia kwenda kupima virusi hivyo. Idadi ndogo ya watu iliropotiwa Mwezi Machi na Aprili ambapo idadi ya waliopima virusi hivyo ilipungua hadi asilimi 33.

Kutokana na hali hiyo, serikali imewahimiza Wakenya kutoaagopa kuvitembelea vituo vya matibabu kutibiwa kutokana na hofu ya kuambukizwa.