×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 11 wafariki dunia kutokana na Covid-19

Watu wengine 11 wafariki dunia kutokana na Covid-19

Wizara ya Afya imesema kuwa taifa linaelekea katika kipindi cha maambukizi ya juu zaidi kati ya Mwezi Agosti na Septemba huku watu wengine kumi na mmoja wakithibitishwa kufariki dunia na kufikisha idadi jumla ya walifariki kutokana na Covid-19 kuwa watu 274.

Katibu wa Utawala wa Wizara ya  Afya Dakta. Mercy Mwangangi amethibitisha kuambukiwa virusi vya korona watu 667 kutokana na vipimo vya sambuli 5,075 vilivyopimwa chini ya kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita. Idadi hii sasa imefikisha jumla ya maambukizi nchini kuwa 16,268 na sambuli 266,102.

Miongoni mwa walioambukizwa 657 ni Wakenya huku kumi wakiwa raia wa mataifa ya kigeni. Mtoto mchanga mwenye umri wa mwezi mmoja na mzee wa miaka 92 ni miongoni mwao.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa visa vya maambukizi ambapo leo hii visa 387 vimeripotiwa, Kiambu 40, Mombasa visa 26, Machakos 47, Kiajiado 79, Nakuru, 15, Uasingishu 14, Garissa 11, Busia 9 , Kilifi na Turkana visa sita sita , Makueni, 5, Wajiri 5 huku Bomet, Narok, Bungoma na Nyamira vikiwa na visa kimoja kimoja.

Watu wengine 311 wamepona huku idadi jumla ya waliopona Covid-19 ikifikia watu 7,446. Miongoni mwao 166 walikuwa wakitibiwa nyumbani huku 145 ni wale waliokuwa wakitibiwa hospitalini.

Wizara ya Afya kwa mara nyingine imewashauri Wakenya kuzingatia maagizo ya kukabili maambukizi hasa taifa linapoekea katika msimu wa maambukizi ya juu katika ya Mwezi Agosti na Septemba.