×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya yaanza majaribio ya kutafuta tiba ya COVID-19

Kenya yaanza majaribio ya kutafuta tiba ya COVID-19

Kenya ni miongoni mwa mataifa mawili Afrika ambayo yameanza majaribio ya kutafuta dawa yakutibu ugonjwa wa COVID-19. Matokeo ya majaribio hayo yanatarajiwa baada ya miezi mitatu ambapo yatabaini iwapo dawa ya  Roche’s medicine Actemra (tocilizumab). Kufikia sasa wagonjwa 10 wamelazwa katika Hospitali ya Aga Khan University hapa jijini Nairobi kuanza majaribio hayo.

Dawa hiyo imetumika katika katika matibabu ya ugonjwa wa nimonia iliyosababishwa na COVID-19 kwa wagonjwa katika taifa la Marekani mwezi Meu kabla ya kuanza kutumika Nchini Kenya, Afrika Kusini, Brazil , Mexico na peru.

Mkurugenzi wa utabibu katika Kampuni ya Roche Daktari Beatrice Nyawira ametaja kufurahishwa na hatua hiyo na kusema kuwa lengo lao ni kuhakikisha suluhu imepatikana. Amesema kuwa ukosefu wa mbinu tofauti za utafiti umelemaza utafiti, akisistiza kuwa Roche itaziba mwanya huo.

Dawa hiyo inatarajiwa kupunguza makali ya protini aina ya Interluekin-6 inayozuia nimonia inayosababishwa na ugonjwa wa COVID-19. Mgonjwa anapoambukizwa virusi vya korona mapafu huanza kupigana na virusi hivyo kwa kutoa kemikali Interluekin-6 inayoua virusi hivyo, hata hivyo vita hivyo vya kinga mwilini huzidi kasi na kusababisha matatizo ya kupumua hivyo kumlazimu mgonjwa kuwekea oksijeni au mashine ya kupumua.

Kwa mujibu wa Prof. Mansoor Saleh, Mkurugenzi katika Kliniki ya Utafiti na Matibabu ya Saratani katika Hospitali ya Aga Khan University, wanadhania kuwa chanzo cha matatizo ya kupumua kunasababishwa na Interluekin-6 , lengo lao ni kuwapa wagonjwa dawa ambayo itaizua kabla ya kuwekwa katika mashine ya kusaidia kupumua.

Kwa muda wa wiki nne Kenya inatarajiwa kuwa na wagonjwa 60 ambao watafanyia majaribio hayo. Baadhi ya wagonjwa hao watapokea dawa hiyo wengine wakipewa placebo ambayo ni njia ya majaribio ambapo wagonjwa hupewa dawa zisizotibu maksudi bila ufahamu wao, huku kundi jingine likipewa dawa hasa zinazofanyiwa majaribio, ili kutathmini tofauti kati ya utendakazi wa dawa na athari za kisaikolojia kuhusu tiba. Aidha kati ya madaktari na wagonjwa hakuna atakayejua aliyepewa dawa kamili au placebo, ili kuhakikisha wote wanapokea huduma sawa.

Asilimia 80 ya wagonjwa watakaofanyiwa majaribio watakuwa na matatizo kidogo ya baadaye au kukosa matatizo kabisa.
Kwa mujibu wa Profes Monsoor , majaribio hayo yalistahili kufanyiwa katika mataifa ya Afrika, kwani dawa inayoweza kufanya kazi Afrika ni tofauti na inayoweza kufanya kazi katika eneo la Amerika Kusini ikizingatiwa hali ya anga ni tofauti.

Aidha, Profesa Mansoor ametaja kufurahishwa na waliojitolea akisema kuwa wengi wao wamesema kuwa majaribio hayo yasipowafaidi basi yatawafaidi madaktari katika utafiti.

Jumla ya wagonjwa 375 wanafanyiwa majaribio hayo katika mataifa mbali mbali.