×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

''Niokoe, Nikuokoe'' -Waziri Kagwe awashauri Wakenya

''Niokoe, Nikuokoe'' -Waziri Kagwe awashauri Wakenya

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameendeela kusisitiza kuwa ni jukumu la kila Mkenya kuhakikisha virusi hivyo havisambai nchini akiwahimiza Wakenya kuzingatia kauli mbiu ya ''Niokoe Nikuokoe''

Wakati uo huo, ametishia kuifunga mikahawa kadhaa jijini Nairobi ambayo inaendelea kukiuka masharti yaliyowekwa na serikali kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.

 

Akizungumza leo hii wakati wa kutangaza takwimu kuhusu maambukizi hayo ya kila siku Waziri Kagwe amesema baadhi ya mikahawa imekuwa ikitumika kama baa, licha ya kuwa maeneo hayo hayajafunguliwa. Amesema mikahawa itakayofungwa aidha itapokonywa leseni za kuhudumu.

Haya yanajiri saa chache tu baada ya Seneta wa Nairobi, Johnson Sakaja ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati maalum ya seneti ya kukabili maambukizi ya korona kukamatwa  katika baa moja kwenye Mtaa wa Kilimani akibugia pombe na watu wengine kumi.

Ripoti ya polisi inaonesha kwamba afisa mmoja wa Kituo cha Polisi cha Kilimani alipokea taarifa mwendo wa saa saba usiku kuhusu kuendelea kuhudumu kwa baa moja kipindi hicho. Baada ya polisi kuelekea huko walimpata Sakaja na watu wengine kumi wakinywa pombe.

 

Ikumbukwe Kenya leo imerekodi idadi ya juu zaidi ya maambukizi ambayo watu mia sita sitini na nane wamethibitishwa kuambukizwa korona katika saa ishirini na nne zilizopita, na kufikisha elfu kumi na mbili mia saba hamsini.

 

Waliopona ni watu mia nne arubaini na saba huku watu wengine watatu zaidi wakifariki dunia.