×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Walio na Kisukari, shinikizo la damu mwilini waongoza katika vifo vya COVID-19

Walio na Kisukari, shinikizo la damu mwilini waongoza katika vifo vya COVID-19

Kufikia sasa imebainika kuwa wanaoathirika pakubwa na virusi vya korona na hata kufariki ni walio na maradhi mengine. Kulingana na ripoti iliyotolewa na Wizara ya afya siku ya Alhamisi tarehe 16 Julai  asilimia 32 ya waliofariki ambao ni watu 38 walikuwa na matatizo ya  shinikizo la damu mwilini pamoja na kisukari. Asilimia 21 ambao ni watu 25 walikuwa na shinikio la damu pekee, asilimia 14 ambao ni watu 16 walikuwa na kisukari pekee.

Vilevile ripoti hiyo inaonyesha kuwa asilimia 9 ambao  ni watu 11 walifariki kutokana na matatizo sugu ya mapafu, mfano, pumu na kifua kikuu. Watu 11 wengine wamefariki kutokana na saratani.

Kinyume na ilivyodhaniwa ni watu wanne tu ambao walikuwa na virusi vya HIV ambao wamefariki kutokana na COVID-19 ambao ni asilimia 3.

Aidha, Watu watano walio na matatizo ya moyo wamefariki dunia kufikia sasa.

Ripoti hiyo vilevile inaonyesha kuwa miongoni mwa Kaunti 42 ambazo zimeripoti visa vya maambukizi ya virusi vya korona ni Kunti 18 pekee ambazo zimeripoti vifo. Kaunti ya Nairobi ikiongoza kwa vifo hivyo ikifuatwa na Mombasa.