array(0) { } Radio Maisha | Bodi ya Madaktari yaagizwa kuchunguza maabara ya Lancet
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Bodi ya Madaktari yaagizwa kuchunguza maabara ya Lancet

Bodi ya Madaktari yaagizwa kuchunguza maabara ya Lancet

Hayo yakijiri, Bodi ya Madaktari imeanza kuichunguza maabara ya binafsi ya Lancet kufuatia malalamiko kuhusu matokeo ya vipimo vya virusi vya korona. Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema aliagiza uchunguzi huo kufanywa kwani kumekuwapo na matokeo yanayokinzana na maabara nyingie au taasisi zilizoidhinishwa kuendesha vipimo hivyo.

Aidha amewashauri wakenya kuepuka kutafuta huduma kutoka kwa maabara ambayo matokeo yake yanaibua maswali.

Waziri Kagwe amesema ni jukumu la serikali kuhakikisha kwamba huduma za afya zinazotolewa nchini ziaafikia viwango vinavyohitajika.

Ameyasema haya siku moja tu baada ya Wafanyakazi kumi na saba wa Shule ya Kimataifa ya St. Andrews Turi iliyoko mjini Molo kwenye Kaunti ya Nakuru waliothibitishwa kuwa na korona baada ya kupimwa katika maabara ya Lancet na kupatikana hawana virusi hivyo walipopimwa tena katika Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu KEMRI.

Kumi na saba hao ni miongoni mwa watu ishirini na wanne waliopimwa Jumatano iliyopita katika Kaunti ya Nakuru kubainisha iwapo wameambukziwa virusi vya korona au la.

Hii si mara ya kwanza kwa baabara ya Lancet kutuhumiwa kutoa matokeo ya korona yanayokinzani na ya hospitali na taasisi nyingine  nchini. Miongoni mwa waliopimwa na Lancet kisha kubainika kuwa wameambukziwa korona ni aliyekuwa mamake mbunge wa Kiambu Jude Njomo hata hivyo vipimo vingine vilivyofanywa katika Nairobi Hospital vilionesha kuwa marehemu hakuwa akiugua COVID-19.

Hali hiyo ilimfanya Njomo kuwasilisha malalamiko mbele ya kamati ya Bunge ya afya.