array(0) { } Radio Maisha | Wizara ya Afya yahofia ongezeko la visa vya korona katika Kaunti ya Nairobi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wizara ya Afya yahofia ongezeko la visa vya korona katika Kaunti ya Nairobi

Wizara ya Afya yahofia ongezeko la visa vya korona katika Kaunti ya Nairobi

Wizara ya Afya imesema inahofia kasi ya ongezeko la visa vya maambukizi ya virusi vya korona katika Kaunti ya Nairobi, huku ikikosoa mienendo ya wakazi wa Nairobi ambao hawazingatii sheria zilizowekwa.Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya Daktari Mercy Mwangangi amesikitishwa na idadi ya maambukizi katika Kaunti ya Nairobi, akisema kwa muda wa siku tatu zilizopita visa 518 vimeripotiwa katika Kaunti hii.

Haya yanajiri huku Kufikia sasa wagonjwa 199 wa COVID-19 wamekuwa katika chumba wa wagonjwa mahututi, miongoni mwao tisini wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku sabini na watatu wakifariki dunia.

Leo vyumba vya wagonjwa mahututi vina wagonjwa 36 pekee, nusu yao ambao ni kumi na wanane wakihitaji mashine za kuwasaidia kupumua, ventilator huku wengine kumi na wanane wakiwekewa oksijeni.

Dkt Patrick Amoth ni Kaimu Mkurugenzi wa Matibabu. kufikia sasa wahudumu wa afya 450 wameambukizwa virusi vya korona. Aidha, amesema miongoni mwao 414 hawana matatizo sugu ya kiafya hivyo hawakuonesha dalili za COVID-19. Hata hivyo miongoni mwao 36 wana matatizo ya kiafya.

Akizungumzia idadi ya walioambukizwa korona kwa muda wa saa ishirini na nne zilizopita, Mwangangi amesema watu mia nne tisini na saba wamethibitishwa baada ya sampuli 4,922 kupimwa. Miongoni mwao mia nne na themanini ni raia wa Kenya huku kumi na saba wakiwa raia wa Kigeni, wote wakiwa kati ya umri wa miaka 2 na themanini na tisa.

Vilevile, watu 71 wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupona idadi jumla y waliopona ikiwa elfu tatu, na kumi na saba, huku watu watano wakifariki dunia idadi jumla ya waliofariki ikiwa mia mbili na mbili.